Ligi KuuNyumbani

Mashujaa kuibuka shujaa leo?

BAADA ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Agosti 15 kushuhudia wageni wa ligi hiyo JKT Tanzania wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo, ligi hiyo inaendelea leo kwa michezo miwili.

Kagera Sugar itakuwa ugenini uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kuikabili Mashujaa ambayo pia imepanda daraja.

‘Wanalambalamba’ Azam ni wenyeji uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ikiwakaribisha wageni wengine wa ligi, Tabora United.

Katika michezo mingine ya ufunguzi Agosti 15, Dodoma Jiji imeichapa Coastal Union mabao 2-1 kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodama wakati Ihefu ikicheza uwanja wa nyumbani wa Highland Estates imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Geita Gold.

Related Articles

Back to top button