Nyota 64 wapikwa SLC
DAR ES SALAAM: VIJANA 64 chini ya umri wa miaka 18, wamepatikana katika michuano ya kombe la Safari Lager iliofanyika Tanzania nzima kwa ajili ya kuibua na kuendeleza vipaji katika sekta ya mpira wa miguu nchini.
Vijana hao, makipa Abubakary Lyanga (Dar es Salaam), Edmund Zephania (Arusha), beki wa kulia, Steven Claudia (Mwanza), beki wa kushoto ni Benson Burton (Dar es Salaam), David Siraji (Arusha), Mathias Anthony, (Dar es Salaam), beki wa kati ni Kisumo Anthony (Mwanza), Jeremiah James (Mbeya),
Baraka Thobias (Mbeya), Augostino Anderson (Arusha), Somji Hailonje (Mbeya), Samson Kamese (Mbeya), Festo Mkumbo (Mbeya), Salim Shida, (Mbeya), Jacob Mussa (Mbeya), Hussein Ally (Dar es Salaam), Kelvin Komba (Mbeya), Habib Kingo (Dar es Salaam), Ibrahim Samweli (Arusha), Erick Ponsian (Arusha), Marwa Mwita (Mwanza) na Prince Paul ,(Arusha)
Kwa mujibu wa Meneja Chapa wa safari Lager, Pamela Kikuli amesema usaili wa mashindano hayo yalifanyika katika majiji ya Mbeya, Arusha, Mwanza, na Dar es Salaam ili kuwapata wanasoka vijana wenye vipaji na wanaoonesha moyo wa mpira wa miguu wa Kitanzania.
Amesema mchujo huo ulikuwa mkali na kambi ya mafunzo yalifanyika na makocha bora huku vijana 64 walihudhuria kwa kuwania nafasi hiyo ya kutafuta bingwa ambapo vijana waliofanikiwa kupita katika mchujo huo wametoka katika nyanja mbalimbali za Maisha.
“Sasa wanaanza kambi ya mafunzo ya wiki tatu chini ya magwiji wa mchezo, wakipata ujuzi wa hali ya juu huku wakionekana katika vyombo vya habari vya kitaifa wakijiandaa kwa mechi moja kubwa ya Mwisho itakayokua ya kihistoria.
Kombe la Safari Lager linaibua vipaji na tunajivunia sana kuzindua timu hii ambayo imepitia changamoto na mchuano mkali ili kuthibitisha ubora wao. Watanzania wote wanapaswa kuwaunga mkono na kuwatambua kama alama za matumaini kwa vijana wengine,” amesema Pamela.
Amesema kliniki hiyo ilitafuta na kupata vijana hao ambao watakuwa muhimili mkubwa kwa miaka ijayo kwa kupata mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa mchezo wa soka.