Ligi Daraja La Kwanza

Tabitha ateuliwa Singida Black Stars

DAR ES SALAAM :UONGOZI wa Singida Black Stars, umetangaza kumteua Tabitha Kidawawa kuwa Mkurugenzi wa Masoko na Mashindano kuanzia leo Februari 19, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mtendaji Mkuu Jonathan Kassano, Kidawawa ana uzoefu wa kutumikia klabu mbalimbali hapa nchini hivyo wana imani na uzoefu wake.

Taarifa hiyo imesema uzoefu wa Kidawawa utakuwa msaada mkubwa katika kuimarisha mikakati ya masoko, kukuza thamani ya chapa ya Singida Black Stars, pamoja na kuboresha ushindani.

“Tunamkaribisha rasmi Kidawawa ndani ya familia ya Singida Black Stars SC na tunamtakia mafanikio mema katika majukumu yake,”imesema.

Kidawawa aliwahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu za Singida Big Star na Fountai Gate.

Related Articles

Back to top button