Azam kushiriki Kombe la Muungano
KLABU ya Azam FC imethibitisha kuwa sehemu ya timu zitakazoshiriki Kombe la Muungano.
Kombe la Muungano litaanza Aprili 23 hadi 27, 2024 visiwani Zanzibar.
“Tunathibitisha tutakuwa sehemu ya timu zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Muungano, itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Aprili 23 hadi 27, 2024, visiwani Zanzibar,” imeeleza taarifa ya Azam.
Septemba 13, 2022 aliyekuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul alisema serikali ilikusudia kurejesha Kombe la Muungano ili kukuza vipaji na kupata wachezaji watakaotumikia timu ya taifa.
Gekul alitoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Suleiman Haroub Suleimanaliyeuliza je, ni vigezo gani vinatumika kuchagua wachezaji wa timu ya taifa.
Akijibu swali hilo Gekul alisema miongoni mwa vigezo ni mchezaji kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mchezaji awe anacheza Klabu ya Ligi za juu, na ufanisi mzuri kiuchezaji, nidhamu ya kiuchezaji na nidhamu ya kawaida pamoja na ufanisi mzuri kiuchezaji.