Mastaa

Steve Nyerere, Shetta, Ommy Dimpoz wamfariji Rais Samia

ZANZIBAR: MSANII Steve Nyerere, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Ali maarufu kwa jina la Shetta, pamoja na wasanii Ommy Dimpoz na Dr Abbas, wamefika Kizimkazi, Zanzibar, kumfariji Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kufuatia msiba wa kufariki kwa mumewe, Hafidh Ameir Hassan.

Walifika kutoa pole na kushiriki katika kumfariji Rais Samia pamoja na familia kufuatia msiba huo.

Steve Nyerere, Shetta, Ommy Dimpoz na Dr Abbas ni miongoni mwa watu mbalimbali wanaoendelea kufika kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi.

Kifo cha Hafidh Ameir Hassan kimeguswa na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi, wasanii na wananchi, ambao wameendelea kutuma salamu za pole na dua kwa Rais Samia na familia nzima.

Related Articles

Back to top button