Mastaa

Jennifer Lopez: Sitafuti mwenza kwa sasa

NEW YORK: MWANAMUZIKI na muigizaji, Jennifer Lopez ameweka wazi kwamba kwa sasa hataki mwenza mpya baada ya talaka yake kutoka kwa Ben Affleck.

Lopez aliwasilisha rasmi talaka mnamo Agosti 20, miaka miwili baada ya harusi yao huko Georgia, ingawa tarehe ya kutengana ilikuwa Aprili 26, 2024.

Katika mwonekano wa hivi majuzi kwenye kipindi cha Nikki Glaser, Lopez hakuonyesha majuto kutokana na kuachana kwao.

“Sitafuti mtu yeyote kwa sasa. Baada ya kila kitu ambacho nimepitia kwa miaka 25 hadi 30 iliyopita, ninajifunza maana ya kuwa peke yangu.

Aliongeza kuwa ingawa maisha yake ya baada ya talaka hayakutokea kama alivyofikiria hapo awali, na hicho ndicho kinachomfanya asitake kuwa na mtu kwa haraka kwa sasa.

Licha ya maumivu hayo, Lopez alisisitiza kwamba hajutii hilo. “Ilikaribia kunivunja moyo, lakini sasa naona kwamba ndicho ninachokihitaji kuwa huru. Ninashukuru kwa nilichojifunza katika ndoa, hata kama ilichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.”

Alipoulizwa kama talaka ilimfundisha chochote, Lopez alisema, “Hatimaye niliipata. Sasa, ninatazamia kufanya Maisha yangu peke yangu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button