Mastaa

Harmonize atoa code ya kurudiana na wapenzi wake wa zamani

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Tanzania, Harmonize, amefunguka kuhusu mahusiano yake ya zamani na kueleza sababu zilizowahi kumfanya kurejea katika mahusiano na baadhi ya wapenzi wake wa zamani.

Harmonize alizungumza hayo katika kipindi cha Obinna TV Extra, ambapo aliulizwa kuhusu historia yake ya kimapenzi, wapenzi wake wa zamani na kama ana mmoja anayempenda zaidi kuliko wengine.

Akijibu swali hilo, msanii huyo alikataa kumtaja mpenzi mmoja wa wapenzi wake wa zamani anayempenda zaidi, akisema anawaheshimu wanawake wote aliowahi kuwa nao katika mahusiano.

Harmonize pia alieleza kuwa kutoa sifa kwa mpenzi wa zamani hadharani kunaweza kusababisha migogoro au wivu, hasa pale ambapo mhusika tayari ameingia kwenye uhusiano mwingine.

Akizungumzia sababu za kurejea kwa baadhi ya wapenzi wake wa zamani, Harmonize alisema wakati mwingine mtu anaweza kuchagua kurudi kwenye uhusiano aliouzoea badala ya kuanza upya na mtu asiyejulikana.

Alisema uamuzi huo unaweza kuchangiwa na hisia, mazoea na hofu ya kuanza maisha mapya na mtu mwingine.

Harmonize alisisitiza kuwa hilo halimaanishi kwamba hawezi kuanzisha uhusiano mpya, akieleza kuwa anaamini muda na Mungu vina nafasi katika kumleta mtu sahihi katika maisha yake.

Akizungumzia kuvunjika kwa baadhi ya mahusiano yake, Harmonize alikiri kuwa kama binadamu amewahi kufanya makosa, huku akisema haoni sababu ya kuwalaumu wapenzi wake wa zamani.
Alisema kila uhusiano aliowahi kupitia umekuwa sehemu ya safari yake ya maisha na umemsaidia kujifunza na kukua.

Related Articles

Back to top button