Kwingineko
Stars kazini FIFA Series leo
TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu(Taifa Stars) inashuka dimbani leo dhidi ya Bulgaria katika mchezo wa mchuano ya FIFA Series 2024 huko Azerbaijan.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Dalga uliopo kitongoji cha Mardakan katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku.
Stars itacheza mechi nyingine ya michuano hiyo Machi 25 dhidi ya Mongolia.