Kwingineko

Mhamasishaji wa Mumbai, Aanvi Kamdar afariki akirekodi

MUMBAI, India: MHAMASISHAJI wa Mumbai Aanvi Kamdar amefariki dunia baada ya kuanguka umbali wa futi 300 kutoka kwenye Maporomoko ya Maji ya Kumbhe alipokuwa akirekodi video kwa kutumia simu katika wilaya ya Raigad ya Maharashtra.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikuwa kwenye matembezi ya monsuni na marafiki zake saba, kwenye maporomoko ya maji huku mvua ikiwa inanyesha.

Polisi wa eneo hilo walisema mwanamke huyo alifariki wakati akifanya video ya mazingira ya kuvutia, aliteleza ndipo alipoanguka kwenye korongo.

Baada ya kuarifiwa na marafiki zake, polisi na waokoaji wa eneo hilo walifika mahali hapo na kumkimbiza katika hospitali ya serikali ya karibu ya Mangaon taluka, ambapo alifariki wakati wa matibabu.

Kamdar alikuwa mhasibu aliyekodishwa na taasisi ya mshawishi wa mitandao ya kijamii ambaye anajulikana kwa kutengeneza video katika mfumo wa reels.

Related Articles

Back to top button