Smokey Robinson hana wasiwasi kwa Lionel Richie

CALIFORNIA: GWIJI wa muziki, Smokey Robinson amewatia moyo mashabiki akiwaeleza kuwa mkongwe, Lionel Richie anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu stahiki.
Richie, 77 kwa sasa amelazwa hospitalini akipatiwa matibabu kwa ajili ya tatizo la mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.
Kwenye mahojiano yake na TMZ, Smokey, 86 alifunguka kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi sababu changamoto aliyonayo Richie hata yeye alikuwa nayo na akapona.
“Rafiki yangu (Richie) anaendelea vizuri sana, na kwamba utaratibu wa kimatibabu aliopitia unaojulikana kama ‘AFib ablation’ ni wa kawaida na wa mara kwa mara, hata mimi nilishawahi kufanyiwa upasuaji huo huo,” alisema.
Pia, alisema hana uhakika na haamini kama Kipindi cha American Idol kitamwondoa Richie kabisa na kumtafuta mtu mwingine kuchukua nafasi yake kama jaji.
Kutokana na changamoto hiyo, Kundi la Earth, Wind & Fire lililazimika kuahirisha shoo zao wanazoshirikiana na Richie, kupisha matibabu yake.
Awali, waliahirisha kwa muda shoo baada ya Richie kwenda hospitalini huko St. Louis baada ya tamasha moja na kisha kufanyiwa vipimo vya moyo mwezi Agosti lakini baadae alipata kizunguzungu wakati akitumbuiza huko St. Paul mwezi Juni, mwaka huu.




