Kompany akubali Arsenal iko vizuri

MUNICH: KOCHA wa Bayern Munich, Vincent Kompany ameitaja Arsenal kama mpinzani wa kiwango cha juu baada ya timu yake kulazimishwa sare ya 2-2 usiku wa jana Jumatano.
Goli la kusawazisha la Declan Rice katika dakika ya 82 lilifanya pambano hilo la Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena kuisha kwa sare.
Arsenal ilitangulia kufunga kwa bao la Eberechi Eze dakika ya 25 kabla ya Alphonso Davies kusawazisha dakika 10 kabla ya mapumziko, na kisha Harry Kane akaipa Bayern uongozi dakika ya 61 kwa mkwaju wa penalti.
“Tulikabiliana na mpinzani imara; tulihisi hilo na kuliona. Nadhani tulikuwa na nyakati zetu nzuri pia.
“Tulipata nafasi kadhaa muhimu ambazo sikutarajia tungezipata. Inasikitisha kidogo, kwa sababu katika dakika kumi hadi 15 za mwisho tuliteseka. Hilo lilipunguza kasi yetu. Bado tulikuwa na imani kuwa tunaweza kushinda mchezo huo, na labda hata tulistahili kushinda.”
“Lakini huyu ni mpinzani imara na mchezo haukuwa umekwisha hadi dakika ya mwisho. Katika wakati huo, lile goli la kusawazisha ni jambo la kusikitisha.
“Arsenal walishinikiza kwa nguvu sawa na sisi. Katika vipindi hivi, tulikuwa hatari. Hatukupata kila mara wakati mwafaka wa kuingia katika theluthi ya mwisho ya uwanja, lakini nadhani tulijikuta katika nafasi hizo mara nyingi zaidi kuliko Arsenal,” alihitimisha Kompany.




