Muziki

Bien:Watanzania wana upendo sana

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki kutoka Kenya, Bien Baraza ‘Bien’, amesema hatasahau mapokezi na mapenzi makubwa aliyooneshwa na Watanzania alipohudhuria fainali ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam kati ya Dar City na Stein Warriors iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Bien, ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaotambulika katika muziki wa Afrika Mashariki, ameeleza hisia zake kupitia ujumbe aliouchapisha leo, akitumia msemo unaosisitiza umuhimu wa ujirani mwema.

“Jirani mwema ni ndugu wa karibu,” aliandika Bien, akionesha namna alivyoguswa na upendo alioupata kutoka kwa Watanzania.

Katika fainali hiyo, Dar City iliibuka bingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupata ushindi wa jumla wa michezo mitatu dhidi ya Stein Warriors, na hivyo kutwaa taji hilo mbele ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano hilo.

Related Articles

Back to top button