Ligi Kuu

Mngqithi: Kazimoto ana nafasi timu ya taifa

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amesema anaamini beki wa kulia, Kazimoto, ana uwezo mkubwa wa kufika mbali katika soka na ana nafasi ya kuitwa katika timu ya taifa kutokana na vipaji alivyonavyo.

Mngqithi amesema alivutiwa na uwezo wa mchezaji huyo tangu alipomwona akicheza nafasi ya beki wa kati, lakini aliona angeweza kufanya vizuri zaidi akitumika upande wa kulia wa ulinzi.

Amesema Kazimoto ana sifa muhimu za kimwili, ikiwamo nguvu, kasi, uwezo wa kucheza mipira ya juu na kukabiliana na wapinzani katika hali ya mchezaji mmoja dhidi ya mmoja.

“Huyu kijana ana mambo mengi mazuri. Ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kucheza mipira ya juu. Kwa maoni yangu, ana nafasi ya kuwa mchezaji wa kiwango cha juu na hata kucheza timu ya taifa,” amesema Mngqithi.

Hata hivyo, kocha huyo amesema Kazimoto bado anahitaji kuboresha maamuzi yake anapokuwa na mpira, akieleza kuwa wakati mwingine hukimbilia kufanya jambo kabla ya kukamilisha pasi.

Kazimoto ni miongoni mwa wachezaji walioifungia Yanga bao katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya CFFA uliochezwa jana na timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Related Articles

Back to top button