Muziki

Mashabiki: Diamond na Zuchu achieni ngoma itikise mitaa 

DAR ES SALAAM:MASHABIKI wa muziki wa Bongo Fleva wamewataka wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zuhura Othumani ‘Zuchu’ kuachia nyimbo mpya zitakazotikisa mitaani, huku wakieleza kutoridhishwa na ukimya wao wa muda mrefu katika kutoa kazi zinazowashirikisha wote wawili.

Baadhi ya mashabiki wameeleza kuwa, licha ya Diamond na Zuchu kushirikiana na wasanii wengine katika nyimbo mbalimbali, bado wanatarajia kuona kila mmoja akitoa wimbo wake binafsi utakaofanya vizuri na kupata umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki.

Miongoni mwa shabiki amesema”Baba na mama Sandra waachie ngoma hit isumbue mitaa yaani chana na zamni tunataka ngoma mpya.” amesema Kitibwisi

Kwa mujibu wa maoni ya mashabiki hao, Diamond na Zuchu wanapaswa kuachana kwa muda na nyimbo za ushirikiano (collabo) pamoja na remix, na badala yake wajikite katika kutoa kazi zao binafsi zitakazothibitisha uwezo wao wa kufanya vizuri bila kumshirikisha msanii mwingine.

Kwa upande wa Zuchu, miongoni mwa nyimbo zake binafsi zilizopata umaarufu ni ‘Amanda’, iliyotolewa mwaka uliopita, huku mashabiki wakiendelea kusubiri kazi nyingine itakayofikia au kuvuka mafanikio ya wimbo huo.

Naye Diamond Platnumz, ambaye ni miongoni mwa majina makubwa katika muziki wa Afrika, anakabiliwa na matarajio ya mashabiki wanaotaka kusikia tena wimbo wake binafsi utakaotawala majukwaa ya muziki na mitaa mbalimbali.

Hata hivyo, maoni hayo yanaibua mjadala kuhusu matarajio ya mashabiki kwa wasanii hao wawili, ambao kila mmoja ana kundi kubwa la wafuasi wanaosubiri kazi mpya zenye uwezo wa kutamba katika soko la muziki.

Swali linalobaki ni je, Diamond Platnumz na Zuchu watajibu kiu ya mashabiki wao kwa kuachia nyimbo binafsi zitakazotikisa mitaani, au wataendelea kuwapa kipaumbele nyimbo za ushirikiano?

Related Articles

Back to top button