FA

Simba yatamba baada ya kufuzu robo fainali

User Rating: Be the first one !

Grace Mkojera

ARUSHA: KLABU ya soka ya Simba kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliono wa timu hiyo, Ahmed Ally amesema Dodoma Jiji sio timu daraja la Simba baada ya ushindi waliopata wa mabao 3-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB.

Simba ni miongoni mwa timu zilizofuzu hatua ya nane bora baada ya kushinda katika mchezo huo ulioochezwa jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Ahmed alisema timu ilicheza kwa kuonesha tofauti ya kiwango kati yake na mpinzani, akibainisha kuwa ushindi huo ulikuwa pia ujumbe kwa wapinzani wao.

“Tumekuja kuwaonesha kwamba ninyi ni Dodoma Jiji mna daraja lenu. Hata mkijikaza vipi sikio haliwezi kuzidi kichwa. Mchezo huu haukuwa tu kushinda, bali kushinda na kuwakumbusha wao ni akina nani,” amesema.

Ameongeza kuwa Simba ilitumia vyema nafasi zake na kucheza mpira wa kiwango cha juu, tofauti na mpango wa Dodoma Jiji uliolenga zaidi kuizuia Simba kuliko kushambulia.

“Dodoma Jiji mpango wao haukuwa kutufunga sisi, bali kutuzuia Simba. Kabla hata hawajafungwa bao, kipa wao alikuwa akipoteza muda. Lakini tumetimiza malengo yetu ya kufuzu robo fainali kwa ushindi wa mabao 3-1,” amesema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button