FANyumbani

Mzunguko wa kwanza ASFC kupigwa leo

MZUNGUKO wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) unapigwa leo kwa michezo nane kufanyika kwenye viwanja tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba, Tanesco itapambana na Machava kwenye uwanja wa Magogo, Kilimanajro wakati Arusha City itakuwa mgeni wa Misitu kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Nyumbu itakuwa mwenyeji wa Malimao kwenye uwanja wa Mabatini, Pwani huku African Lyon ikiwa mgeni wa Kilosa United kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mechi nyingine Tanzania Navy itakuwa ugegeni kuivaa Eagle kwenye uwanja wa TFF, Kigamboni Dar es Salaam wakati Bunda Kids itakuwa nyumbani uwanja wa Karume mkoani Mara kuikaribisha Damali.

Mbao itakuwa mwenyeji wa Bilo kwenye uwanja wa Taifa, Shinyanga wakati Green Land itakuwa mgeni wa Geita Academy kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Related Articles

Back to top button