Nyumbani

Dullah Mbabe apewa baraka Kisarawe

DAR ES SALAAM: Bondia Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe amepewa baraka na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, kuelekea pambano lake la Dar Boxing Derby dhidi ya Hussein Itaba litakalofanyika Julai 24, 2026 Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kumuaga bondia huyo katika Ofisi ya Wilaya ya Kisarawe, Magoti amesema ana imani kubwa na Dullah Mbabe kutokana na maandalizi aliyofanya akiwa kambini wilayani humo, akiamini ataibuka na ushindi katika pambano hilo.

Amesema ataunga mkono safari ya bondia huyo na amepanga kufika ukumbi wa EACC Dar es Salaam kushuhudia pambano hilo la kihistoria.

Kwa upande wake, Dullah Mbabe amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa sapoti na mazingira mazuri aliyoyapata wakati wa maandalizi, huku akiahidi kulipa kwa ushindi wa mtoano (KO).

Katika pambano kutakuwa na mapambano zaidi ya 10 na miongoni mwao watakaokuwepo ni Debora Mwenda, Juma Choki na Tony Rashidi.

Related Articles

Back to top button