Neddy: Si kila Kitu kinapaswa kuwekwa hadharani

DAR ES SALAAM: Msanii wa muziki, Neddy, amewataka watu kuwa waangalifu kuhusu mambo wanayoyaweka hadharani, akisisitiza kuwa si kila jambo linapaswa kufahamika na kila mtu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, msanii huyo ameandika kuwa mara nyingi watu hawawezi kushambulia kitu ambacho hawakijui, hivyo ni muhimu kulinda siri na mafanikio binafsi.
“Niliwahi kusikia mwenye hekima mmoja akisema, ‘People Can’t Attack What They Don’t Know,’ yaani watu hawawezi kushambulia kitu ambacho hawakijui,” ameandika.
Neddy ameongeza kuwa kuna watu ambao mwanzo wa matatizo yao ulitokana na kuweka hadharani mambo yaliyopaswa kubaki siri.
Amesisitiza kuwa baadhi ya taarifa zinapaswa kulindwa kama ilivyo password ya kadi ya benki, huku nyingine zikitakiwa kufichwa kwa muda na kuoneshwa pale wakati sahihi utakapofika.
Aidha, amesema watu wengi hawajawa maadui wa wengine kwa sababu bado hawajui kila kitu walichonacho au kinachowapa furaha, akionya kuwa baadhi wanaweza kubadilika na kuwa chanzo cha matatizo pindi wanapopata taarifa ambazo hawakupaswa kuzijua.
Amehitimisha ujumbe wake, Neddy Fire Boy amewahimiza wafuasi wake kutumia busara katika kuamua ni mambo gani waweke wazi na ni wakati gani wa kufanya hivyo, akisema uchaguzi sahihi wa kile cha kuonesha unaweza kuwa kinga dhidi ya changamoto zisizo za lazima.




