Ligi Kuu
Simba yampa raha Mo Dewji
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji amewapongeza wachezaji wat imu hiyo na kudai wanaendelea kujenga safari ya mafanikio ya klabu hiyo.
Mo Dewji ameonesha kurufahishwa na ushindi Simba katika michezo mitatu mfululizo ya Ligi Kuu Tanzania Bara lakini pia kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram amesema, “ushindi dhidi ya Azam FC! Hongera kwa wachezaji wetu kwa kujituma na kuonesha moyo wa ushindi,”.
Ameeongeza kuwa bado wanaendelea kujenga kikosi cha timu hiyo kuwa imara na tishio kwa kurejesha heshima yao ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.