Yanga yaweka ngumu, hakuna Dabi

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Yanga umesema hakuna kilichobadilika katika maamuzi yao ya awali licha ya jana kuwa na kikao na Waziri wa Habari, Utaamdani, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema tangu jana Rais wa Yanga Hersi Said alisisitiza kuwa kikao cha jana hakikuwa cha maamuzi ya dabi bali kilikuwa ni kwaajili ya kuwasikiliza yale waliyonayo hivyo hakukuwa na maamuzi yoyote.
Kamwe amesema kile kilichoamuliwa awali kuwa hawatoshiriki tena mchezo wa Dabi ya Karikioo kinaendelea kusimama kama msmamo wao kwani hata wanachama na mashabiki wao wanawaunga mkono.
Amesema tayari klabu hiyo imefunga rasmi ukurasa wa Dabi ya Kariakoo na sasa wanaendelea na taratibu nyingine.
Ikumbukwe kuwa mashabiki wa soka nchini bado wana kiu ya kuona ni nini hatma ya mchezo huo baada ya kuahirishwa Machi 8 mwaka huu na hadi sasa bado hali haijatulia.