
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga ameahidi kuendeleza mapambano ili kubaki kwenye nafasi tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara hadi mwisho wa msimu.
Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema ili kufikia malengo mikakati ni kushinda mechi nane hadi 10 kwenye mzunguko wa kwanza.
“Ni kweli ligi imekuwa ngumu na ushindani ni mkubwa lakini lengo letu msimu huu ni kumaliza ndani ya nafasi tatu za juu kwetu hili linawezekana,” amesema Mayanga.
Amesema anaamini lengo litatimia endapo watafanikiwa kushinda idadi kama hiyo ya michezo katika mzunguko wa pili.
Mtibwa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 9.