Simba Queens yautaka ubingwa wa Samia

KOCHA Mkuu wa Simba Queens Yussif Basigi amesema wako tayari kupambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kombe la Samia.
Akizungumzia mchezo wake wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya JKT Queens utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha amesema wanajua wanacheza na timu bora kama JKT Queens na wapo tayaru kupambana.
“Nimpongeze Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha michuano hii kwa ajili ya timu za wanawake tupo hapa kupambana na kuhakikisha tunachukua ubingwa,”amesema.
Nahodha wa Simba Queens Violeth Nicholaus amesema wamejiandaa vizuri na kuahidi kuwa wanahitaji kushinda na kufika fainali na ikiwezekana kuondoka na ubingwa.
Kocha wa JKT Queens Ester Chabruma amesema:”Tunashukuru kuwa timu moja wapo kwenye mashindano aya , tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu wa kesho , Simba Queens ni timu nzuri lakini JKT Queens ni timu nzuri zaidi,”
“Sisi benchi la ufundi tumeiandaa vizuri timu yetu tunaamini wachezaji watafanyia kazi maelekezo ya walimu na kuweza kupata ushindi katika mchezo huu,”amesema.