Nyumbani
Kuna nini Simba na Mayele?
MSHAMBULIAJI wa Pyramids FC, Fiston Mayele atembelea hoteli ilipofikia Simba SC, jijini Cairo Misri.
Katika video fupi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amemkaribisha nyota huyo hotelini hapo.
Timu hiyo ipo Misri kucheza mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly hapo kesho saa 5:00 usiku.
Mayele aliwahi kucheza Yanga ambapo msimu uliopita aliondoka na kujiunga na timu hiyo ya Misri.