Tetesi

Sancho kutimka Man Utd

WINGA wa Manchester United Jadon Sancho anatarajiwa kuondoka klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la uhamisho Januari, 2024 baada ya kushindwa kumaliza tofauti yake na kocha Erik ten Hag.

Sancho amefanya mazungumzo na Ten Hag kuhusu hatma yake United kufuatia kurushiana vijembe kati yao.

Ten Hag alimwondoa winga huyo wa England kwenye kikosi kilichopokea kwa kipigo hivi karibuni toka kwa Arsenal na akieleza mtazamo mbaya na uvivu kwenye mazoezi wa Sancho kuwa ndio sababu za maamuzi hayo.

Sancho alijibu kupitia mitandao ya kijamii akikanisha madai hayo na kumshutumu Ten Hag kwa kusema uongo.

Rpoti zimesema hata kukosekana kwa sasa kwa winga mwenzake Antony kutokana na madai ya unyanyasi wa nyumbani ambayo amekanusha, hakutarajiwi kuongeza nafasi ya Sancho kurejea kikosi cha kwanza.

Manchester United ilimsajili Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 22 mwaka 2021 kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho ya dola milioni 87.94 sawa na shilingi bilioni 215.

Related Articles

Back to top button