Nyota ya Osimhen yaendelea kung’ara
TETESI za usajili zinasema Chelsea ina hofu itamkosa mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen,25, majira yajayo ya kiangazi, huku Paris Saint-Germain na Arsenal zikiongoza mbio za kumsajili mshambuliaji huyo anayewindwa na klabu nyingi kwa udi na uvumba. (Teamtalk)
Fowadi wa Manchester United Marcus Rashford, 26, hatarajiwi kuhamia PSG majira yajayo ya kiangazi kufuatia ripoti kwamba mwingereza huyo atachukua nafasi ya mshambuliaji wa kifaransa Kylian Mbappe, 25. (Sky Sports)
Getafe haitaweza kumbakiza Mason Greenwood,22, zaidi ya kipindi chake cha mkopo baada ya Manchester United kuamua kumuuza fowadi huyo wa England kwa ofa ya juu zaidi ikianzia pauni mil 42.7. (Marca – in Spanish)
Manchester City imeamua kuahirisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa kiungo mbelgiji Kevin de Bruyne, 32, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake. (Football Insider)
Chelsea inamwania beki wa Bournemouth Milos Kerkez, 20, lakini inakabiliwa na ushindani toka Manchester United kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Hungary. (Mirror)