Tetesi

Mbappé ‘kukiwasha Liverpool’

TETESI za usajili zinaeleza kuuzwa kwa fowadi wa Misri, Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 31 majira yajayo ya kiangazi kunaweza kutoa nafasi kwa Liverpool kumsajili fowadi wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappé mwenye umri wa miaka 23.(Team Talk)

Mbappé bado ana mkataba PSG msimu huu na hakuna dalili ya nia kutoka Liverpool.(Football Transfers)

Aston Villa ipo tayari kupokea ofa kumsajili kiungo mbelgiji, Leander Dendoncker mwenye umri wa miaka 28, ambaye anafuatiliwa na Everton.(Football Insider)

Everton na Crystal Palace zina nia kumsajili kiungo wa Ireland anayecheza Leicester City, Kasey McAteer mwenye umri wa miaka 22.(Football Transfers)

AC Milan inaangalia uwezekano wa kuimarisha eneo la ulinzi wa kati kwa kumsajili kwa mkopo beki wa Poland, Jakub Kiwio anayecheza Arsenal mwenye umri wa miaka 23, Januari 2024.(Calciomercato – in Italian)

Newcastle ina nia kumsajili mshambuliaji wa Guinea anayekipiga Stuttgart, Serhou Guirassy, mwenye umri wa miaka 27.(Rudy Galetti)

Related Articles

Back to top button