Tetesi

Salah akibaki, Diaz atauzwa Liverpool

TETESI za usajili zinasema Liverpool itajiandaa kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza fowadi raia wa Colombia Luis Diaz, 27, majira yajayo ya kiangazi iwapo fowadi raia wa Misri Mohamed Salah, 31, atakubali mkataba mpya.(Sun)

Liverpool itataka ada ya zaidi ya pauni mil 100 kumuuza Salah Ligi ya kulipwa Saudi Arabia majira yajayo ya kiangazo ili kupata fedha za zitakazotosha kununua mchezaji mbadala. (Football Insider)

Tottenham Hotspur inaendelea kufuatilia hali ya Conor Gallagher wa Chelsea,24, na ipo tayari kuangalia uwezekano wa kumsajili majira yajayo ya kiangazi. Hata hivyo, kiungo huyo wa England msimamo wake ni kupigania nafasi Stamford Bridge licha ya majadiliano kuhusu mkataba mpya kukwama. (Daily Mail)

Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis amesema hawezi kuwazuia wachezaji kama mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen, 25, kuondoka klabu hiyo majira yajayo ya kiangazi lakini anasema kipengele cha kuachiwa cha mshambuliaji huyo ni cha “fedha nyingi”. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain itakabiliana na ushindani toka Manchester City, Manchester United, Newcastle United, Liverpool na Tottenham Hotspur katika mbio za kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Joshua Kimmich.(HITC)

Kwa Man City, Kimmich anaweza kuwa mbadala wa Mateo Kovacic, ambaye huenda akaondoka kwenda Saudi Arabia majira yajayo ya kiangazi. (HITC)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button