Tetesi

Liverpool, Real Madrid vinara kumwania Leao

TETESI za usajili zinadai Liverpool na Real Madrid zinaongoza katika kuwania saini ya winga wa AC Milan, Rafael Leao, ambaye anakadairiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 130 sawa na shilingi bilioni 391.4. (Fichajes)

Borussia Dortmund inatafuta mnunuzi wa mshambuliaji Youssoufa Moukoko mwenye umri miaka 18. Mawasiliano yamefanyika na Barcelona, Chelsea, Liverpool, Juventus na Real Madrid kwa ada ya pauni milioni 30. (Defensa Central)

Kati ya vilabu hivyo Chelsea ipo tayari kutoa ofa ya pauni milioni 26 kumsajili Moukoko Januari, 2024.(Fichajes)

Manchester United ipo tayari kumuuza Jadon Sancho Januari, 2024 na itakubali hasara kubwa kutokana kumnunua mchezaji huyo kutoka Dortmund kwa pauni milioni 73.(Star)

Barcelona tayari inafahamu gharama za kuwasajili Joao Felix na Joao Cancelo kwa mikataba ya kudumu. Atletico Madrid itahitaji pauni milioni 69 kwa ajili ya Felix huku Manchester City ikitaka ada ya pauni milioni 22 kwa ajili ya Cancelo.(Mundo Deportivo)

Baada ya Manchester City kuonesha nia majira ya kiangazi, Crystal Palace inajiandaa kufungua mazungumzo ya mkataba na kiungo Ebere Eze.(The Athletic)

Hugo Lloris anatarajiwa kuondoka Tottenham Hotspur akiwa huru Januari, 2024 baada ya kushindwa kupata timu mpya majira ya kiangazi.(Telegraph)

Related Articles

Back to top button