EPL

Salah achagua kati ya EPL na UCL

LIVERPOOL:Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ametangaza wazi kuwa anapendelea kushinda taji la Ligi Kuu ya England (EPL) kuliko Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu huu.

Salah, ambaye tayari amewahi kushinda mataji yote mawili akiwa na Liverpool, amekuwa katika kiwango bora msimu huu chini ya kocha mpya, Arne Slot. Kufikia sasa, amefunga mabao 17 na kutoa pasi za mabao 13 kwenye EPL msimu huu.

Liverpool kwa sasa wanaongoza msimamo wa EPL wakiwa na pointi 45 baada ya mechi 18, na wanajiandaa kuivaa Manchester United wikendi hii.

Akizungumza na TNT Sports kabla ya mchezo huo, Salah alisema:
“Nataka kushinda taji la Ligi Kuu zaidi kuliko Ligi ya Mabingwa mwaka huu. Ninalitamani sana, na kama timu tunalitamani pia.”

Related Articles

Back to top button