Diaz: tunataka kila taji
LIVERPOOL, ENGLAND: Kiungo wa majogoo wa jiji la Liverpool, Luis Diaz amesema yeye na wachezaji wenzake wa klabu hiyo ‘watawinda kila kilicho mbele yao’ akimaanisha watapambana kushinda kila kombe ambalo mabingwa hao wa zamani wa Ligi kuu ya England wanashiriki.
Diaz amekiambia kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England katika mahojiano maalumu na kituo hicho kuwa ni malengo yao kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya England, Ligi ya mabingwa barani Ulaya na michuano yoyote ambayo Liverpool wanashiriki.
“2023/24 ulikuwa msimu mgumu sana. Lakini msimu huu nina uhakika wa asilimia 100. Lazima niwe bora zaidi. Pia tunapaswa kuwa bora kama timu. Tunatumai tunaweza kufikia kila kitu ambacho tunakusudia kufanya. Msimu huu tunataka kushinda na kufanya vizuri kwenye kila tunachoshiriki”, amesema Diaz.
Msimu huu Luis Diaz amecheza mechi 5 za ligi kuu ya England akifunga mabao matano na ‘Asisti’ moja na ni mfungaji namba mbili nyuma ya Erling Haaland wa Manchester city.