Rais Samia Atoa neno kwa wanasimba
DAR ES SALAAM: RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi mashabiki wa Klabu ya Simba kusahau yaliyopita msimu wa 2023/24 na kujikita na msimu mpya wa mashindano wa 2024/25.
Samia ameipongeza klabu hiyo kwa maandalizi mazuri ya tamasha la Simba Day ambalo wamefanikiwa kwa asilimia kubwa.
Rais aliwahi kuwa mgeni rasmi simba Day iliyopita, kauli hiyo ameongea baada ya kupiga simu kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, wakati Simba ilipomaliza utambulisho wa wachezaji wa Simba katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji, amesema anapenda kutoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya.
“Napenda kulishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu, Tff na bodi ya Ligi Kuu ya bara kwa ushirikiano wao thabiti wanaoufanya kuinua mpira wetu, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji Simba kwa kazi nzuri wanayoifanya kuipambania klabu,” amesema Mo Dewji.