Nyumbani
Ligi ya mabingwa mikoa Machi 8
MASHINDANO ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL2024) hatua ya makundi inatarajiwa kuanza Machi 8, 2024.
Taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema ligi hiyo ya mkondo mmoja itachezwa katika vituo vinne vitakavyokuwa na timu saba kila kituo.
Makundi, timu na vituo ni kama ifuatavyo:
KUNDI A: NJOMBE
Hausing, Tutes Hub, Don Bosco, Tukuyu Stars, Mkwajuni, THB na Polisi Katavi.
KUNDI B: PWANI
Kiduli, Black Six, Red Angels, Stand, Moro Kids, Gunners na Singida Clusters.
KUNDI C: MANYARA
Reggae Boys, Arusha City, Kawele, Veteran Middle Age, Mabao, Maswa na Eagle.
KUNDI D: MWANZA
Rock Solutions, Bweri, Bukombe Combine, Leo Tena, Mambali Ushirikiano, Kandahari na Rangers.