Tetesi

PSG yataka saini ya Rashford

TETESI za usajili zinasema klabu ya Paris Saint-Germain inaandaa ombi la pauni mil 80 kumsajili fowadi wa England anayekipiga Manchester United,  Marcus Rashford, 26, na itakuwa tayari kumlipa pauni 500,000 kwa wiki. (Star)

Timu ya usajili ya Manchester United inafanya ziara katika vilabu vikubwa zaidi Ulaya kabla ya dirisha la usajili ikiwa ni juhudi za kuanza mapema kukijenga upya kikosi cha timu hiyo. (ESPN)

PSG ina nia kumsajili winga wa Colombia anayecheza Liverpool Luis Diaz, 27, awe mbadala wa fowadi wa kifaransa Kylian Mbappe, 25, ambaye anatarajiwa kujiunga na Real Madrid. (El Pais – in Spanish)

Brighton inazidi kupata hofu kuwa kocha mkuu wa kbalu hiyo Roberto de Zerbi ataondoka majira yajayo ya kiangazi kufuatia Barcelona, Chelsea na Liverpool kuonesha nia kumteua. (Times – subscription)

Liverpool ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England zenye nia kumsajili fowadi mjerumani wa timu ya Hoffenheim, Maximilian Beier,21.(Bild via Express)

Arsenal inataka kumsajili golikipa wa Columbus Crew na Marekani Patrick Schulte, 23, iwapo golikipa wa England Aaron Ramsdale, 25, ataondoka majira yajayo ya kiangazi. (Telegraph – subscription)

Related Articles

Back to top button