Tetesi

Newcastle kumuuza Guimaraes

TETESI za usajili zinasema Newcastle United itafikiria kumuuza kiungo mbrazil Bruno Guimaraes, 26, kugharamia matumizi majira yajayo ya kiangazi. (Football Insider)

Real Madrid na Paris Saint-Germain walikuwa wakimwangalia Guimaraes katika mchezo wa Kombe la FA klabu yake ilipopokea kichapo cha mabao 2-0 toka Manchester City Machi 16, wakati pia PSG inafuatilia kwa karibu mchezaji mwenzake wa Newcastle mshambuliaji wa kisweden Alexander Isak, 24. (HITC)

Bayern Munich ipo tayari kumuuza kiungo mjerumani Joshua Kimmich majira yajayo ya kiangazi lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anapenda tu kujiunga na Manchester City, Arsenal, Liverpool, Real Madrid au Barcelona. (Florian Plettenberg)

Manchester United na Liverpool ni miongoni mwa vilabu vyenye nia kumsajili fowadi wa Morocco anayecheza Real Madrid, Brahim Diaz, 24. (HITC)

Everton itataka pauni mil 80 toka kwa timu itayomhitaji beki wa England, Jarrad Branthwaite, 21, ambaye anawindwa na Manchester United na Chelsea. (Teamtalk)

Huenda Eddie Nketiah akaondoka Arsenal majira yajayo ya kiangazi na Wolves imejiunga na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England kufukuzia dili la mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Teamtalk)

Related Articles

Back to top button