Tetesi

Osimhen chaguo namba 1 kumrithi Mbappé

KLABU ya Paris Saint-Germain imeripotiwa kumchagua mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen kuwa mrithi wa Kylian Mbappé atakapoondoka klabu hiyo majira yajayo ya kiangazi.

Mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappé (Picha:www.thetimes.co.uk)

Wiki hii Mbappé, 25, amewaambia mabingwa hao wa Ligue 1 kwamba hataongeza mkataba wake zaidi ya mwisho wa msimu huu.

Tayari mkazo umeelekezwa kwa nani anayeweza kuziba pengo la Mbappé, na Osimhen anaongoza orodha ya PSG.

Hata hivyo dili la Osimhen huenda lisiwe rahisi huku Napoli ikiwa imeweka thamani ya nyota huyo wa Nigeria kuwa pauni mil 130.

Amekuwa akihusishwa kuhamia Ligi Kuu England huku Chelsea na Arsenal zikiripotiwa kufuatilia hali yake.

Mwezi uliopita Osimhen aliweka bayana kwamba tayari amefanya maamuzi kuhusu hatma yake na anatarajiwa kuondoka Napoli majira yajayo ya kiangazi licha ya kuwa na mkataba na klabu hiyo ya Serie A unaofikia kikomo 2026.

Osimhen, 25, alichangia kwa kiasi kikubwa ubingwa wa Napoli msimu uliopita akifunga magoli 26 katika michezo 32 klabu hiyo ilipotwaa taji la kwanza la ligi kwa miaka 33.

Related Articles

Back to top button