Filamu

Priyanka Chopra aingia kwenye filamu za vichekesho

NEW YORK: MUIGIZAJI nguli kutoka India Priyanka Chopra na Michael Peña wametangaza kuja na filamu mpya ya vichekesho.

Priyanka alithibitisha kuhusika kwake katika mradi huo kwa kushiriki picha ya siri ya tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kuzua gumzo miongoni mwa mashabiki wake.

Muigizaji huyo ameungana tena na muigizaji mwenzake wa Baywatch Zac Efron kupitia kampuni ya utayarishaji filamu ya Amazon MGM Studios. Imetayarishwa na Will Ferrell, Jessica Elbaum na Alex Brown kwa Gloria Sanchez Productions na Nicholas kwa Stoller Global Solutions.

Mume wa Priyanka Chopra, Nick Jonas amesema Chopra atajiunga na waigizaji nyota wa vichekesho nyota Regina Hall, Jimmy Tatro na Billy Eichner.

Filamu hiyo awali iliitwa ‘Siku ya Hukumu’. Inaangazia mfungwa mchanga amnbaye anacheza Zac Efron ambaye anatoka gerezani na kuchukua mateka wa chumba cha mahakama cha TV kwa sababu ana hakika kwamba hakimu ambaye ni Will Ferrell alitoa uamuzi ulioharibu maisha yake.

Related Articles

Back to top button