
MUANDAAJI wa tamthilia ya Toboa Tobo, Devotha Mayunga ameshauri waigizaji na waandaji wa filamu ni vyema kuwapunguzia majukumu watu wengine ili kuleta ufanisi katika kila wanachokifanya.
Devotha Mayunga ambaye pia ni mwandishi wa stori za filamu amesema mtu mmoja kuwa na majukumu mengi kunapunguza ufanisi wa kazi.
“Upande wangu nafikiri ni bora kugawa majukumu kuwapa na watu wengine, ili kuwe na ujumuishaji wa mawazo, kuliko kuwa na mtu mmoja, kwasababu unavyokuwa na mtu mmoja, mzalishaji, mwandishi na muongozaji huyo huyo, maana yake manaishi kwenye mawazo ya mtu mmoja,” amesema Devotha.
Amesema kwa kufanya hivyo kutaboresha utendaji wa shughuli za kuongoza na kuzalisha filamu na kuwa na kiwanda chenye ubora.