Pete ya uchumba ya Careen yaacha maswali

DAR ES SALAAM: MREMBO na mwanamitindo , Caren Simba, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuchapisha picha zake akiwa amevalishwa pete inayodhaniwa kuwa ya uchumba.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Caren ameonekana akiwa na furaha huku akionesha pete hiyo, jambo lililowafanya mashabiki na wadau wa mitandao ya kijamii kuanza kujiuliza kuhusu hatua hiyo mpya katika maisha yake.
Hata hivyo, hadi sasa Caren Simba hajaweka wazi ni nani aliyemvalisha pete hiyo, hali iliyoongeza sintofahamu na mjadala miongoni mwa wafuasi wake.
Baadhi ya mashabiki wamejitokeza kumpongeza kwa hatua hiyo, huku wengine wakisubiri kwa hamu kupata ufafanuzi zaidi kuhusu mchumba huyo asiyejulikana.
Hatua hiyo imefanya mashabiki wa mtandaoni, wengi kutaka kujua ukweli na hatima ya uhusiano huo mpya wa mrembo huyo.




