Nyumbani

Pedro awatia moyo wachezaji wake, awapongeza

ZANZIBAR:KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves ameonesha kujivunia kikosi chake licha ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Simba katika fainali ya Kombe la Muungano, akisisitiza kuwa timu ilipambana hadi mwisho wa mashindano hayo.

Pedro amesema anajivunia namna wachezaji walivyoonesha kujitoa, umoja na morali ya hali ya juu katika michuano yote, akibainisha kuwa hayo ni mafanikio muhimu kwa timu licha ya matokeo ya mwisho kutokuwa upande wao.

Aidha, amewashukuru mashabiki wa Yanga (Wananchi) kwa sapoti kubwa waliyoitoa, akisema imekuwa chachu kwa timu kila hatua.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo ujao wa Jumapili pamoja na kuendeleza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, ambapo Yanga ipo kileleni nafasi wanayoamini wameipata kwa juhudi zao wenyewe na wanapaswa kuilinda kwa kupambana zaidi.

Amesisitiza umuhimu wa mashabiki kuendelea kuwa pamoja na timu, akieleza kuwa sapoti yao itakuwa silaha muhimu katika safari ya kuelekea mafanikio.

Yanga ina kibarua kingine kizito Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ambapo itakutana tena na Simba kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo, mchezo wa jasho au damu katika mbio za ubingwa.

Mwisho

Related Articles

Back to top button