
BEKI wa Azam Malickou Ndoye amesaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Dar es Salaam.
Wachezaji wengine walioongeza mikataba yao Azam tangu Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/2023 kufikia tamati ni Daniel Amoah, Nathaniel Chilambo, James Akaminko na Sospeter Bajana.
“Ndoye, ambaye ameungana na kocha wake wa zamani, @youssouph_dabo, atayeifunza klabu yetu kuanzia msimu ujao, amesaini mkataba huo utakaomfanya kudumu Azam Complex hadi mwaka 2025,” imesema taarifa ya Azam kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Ndoye raia wa Senegal alijiunga na Azam Julai 19, 2022 akitokea Teungueth ya nchi hiyo.