Nyumbani

Zimbwe JR: Indonesia hawatusumbui

JAKARTA. BEKI wa timu ya Taifa Stars, Mohammed Hussein ‘Zimbwe JR’, ameahidi kufanya vizuri kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Indonesia, ukiwa mchezo maandalizi kuwania kufuzu ushiriki wa kombe la Dunia dhidi ya Zambia.

Stars kabla ya kuvaana na Zambia Juni 2,2024 itacheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao kwenye uwanja wa Gelora Bung Karmo,Indonesia utakaopigwa saa sita mchana. Hivi karibuni Stars walicheza mechi mbili za kirafiki na Sudan na kutofanya vizuri baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 na sare ya 1-1, michezo yote miwili uliochezwa, Saudi Arabia.

Akizungumza na Spotileo, Zimbwe JR amesema hivi karibuni hawakufanya vizuri katika mechi za kirafiki sasa wamesahihisha makosa na kupambana kutafuta matokeo mazuri katika mchezo wao wa Jumapili.

Amesema maandalizi yanaendelea vizuri benchi la ufundi linaendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na kupambana kutafuta matokeo mazuri katika mechi dhidi ya Indonesia.

“Hatukuwa na matokeo mazuri michezo miwili ya mwisho na tunaenda kufanya vizuri dhidi ya Indonesia na tutafuata maelekezo tuliyopewa na benchi la ufundi, hii mechi ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu wa kutafuta kufuzu ushiriki wa kombe la dunia dhidi ya Zambia,” anasema beki huyo.

Juni 11, mwaka huu Stars inatarajia kucheza mchezo huo wa kundi E, kwa ajili ya kufuzu kombe la Dunia 2026, mchezo utakaopigwa uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.
Michuano ya Kombe la Dunia 2026 inatarajia kufanyika katika nchini Marekani, Canada na Mexico ambapo timu tisa kutoka Afrika ndio zitakazofuzu.

Tayari Stars imecheza mechi mbili za kundi hilo ikianza kushinda 0-1 ugenini dhidi ya Niger Novemba 18, mwaka jana, uwanja wa Marrekech nchini Morocco bao pekee la Charles M`Mombwa.

Mechi ya pili iliyochezwa nyumbani, Novemba 21, 2023, Stars ilikubali kichapo cha mabao 2-0 na Morocco kwenye uwanja wa Benjamini, Mkapa, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button