Filamu

KFPA walalamikia kuporomoka kwa soko la filamu zao

INDIA: CHAMA cha Watayarishaji wa Filamu za Kerala (KFPA) kimeripoti kwamba kati ya filamu 17 za Kimalayalam zilizotolewa mwezi uliopita, ni filamu moja tu ndiyo iliyovuma.

Chama hicho kimesema licha ya filamu hizo kuporomoka katika soko la filamu Kimalayalam, ni filamu moja tu iliyovuma na kukusanya rupia 10,000 pekee.

Makamu wa rais wa KFPA, G Suresh Kumar aliwaambia waandishi wa habari, kuwa filamu hizo 17 na moja tu kufanya vizuri zilitolewa mwezi Februari.

“Kati ya filamu 17 zilizotolewa Februari, kulikuwa na filamu moja tu, lakini sinema mbili, ikiwa ni pamoja na ‘Daveed’ na ‘Bromance’, haziwezi kupata hasara, kwani zinaweza kufidia pengo la ushiriki wa maonyesho kupitia uuzaji wa OTT na haki zingine.” Amesema Kumar akifafanua hali hiyo ya filamu kudorora sokoni.

Kulingana na chama hicho, jumla ya bajeti ya filamu zilizotolewa mwezi wa Februari ilikuwa ni karibu rupia 75.23 crore, na jumla ya hisa katika makusanyo ya uigizaji ilikuwa rupia 23.55 crore pekee.

Makamu war ais huyo ameongeza kuwa mnamo Januari, walirekodi hasara ya rupia 110 crore katika filamu 28 zilizotolewa mwezi huo.

Related Articles

Back to top button