Kwingineko

Paris kusaidia wafanyabiashara wanawake

LOS ANGELES: Mjasiriamali na nyota wa burudani Paris Hilton amezindua mfuko maalumu wa kusaidia wanawake wamiliki wa biashara ndogo waliokumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo moto.

Hilton ametoa dola 350,000 kuanzisha mfuko huo uitwao ‘Back in Business Recovery Fund’ kwa kushirikiana na taasisi ya GoFundMe.

Paris amesema lengo la mfuko huo ni kukusanya angalau dola milioni moja hadi mwisho wa mwezi Machi.

Anasema anafanya hivyo ili kuwasaidia wanawake kurejesha biashara zao baada ya majanga mbalimbali, yaliyowakumba ikiwemo janga la moto mkubwa uliotokea mwaka 2025 huko Los Angeles.

Related Articles

Back to top button