Kwingineko

Brighton yawinda saini ya Matvienko

TIMU ya Brighton & Hove Albion inaangalia uwezekano wa dili la kumsajili beki wa kati wa Shakhtar Donetsk, Mykola Matvienko.

Matvienko mwenye umri wa miaka 26 amekuwa muhimu katika safu ya ulinzi ya Shakhtar kwa miaka kadhaa huku pia akiwa amecheza Mechi 52 timu ya taifa ya Ukraine tangu alipoitwa kikosi cha wakubwa mwaka 2017.

Mtandao wa soka, 90min, umesema Brighton ambayo sasa inafundishwa na
kocha wa zamani wa Shakhtar, Roberto De Zerbi iko katika mazungumzo kuhusu dili hilo.

Shakhtar inataka ada isiyopungua ada ya Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 63 ingawa kwa sasa Brighton inasita kulipa zaidi ya Euro milioni 15 sawa na shilingi bilioni 37.8.

Klabu nyingine za Ligi Kuu England Brentford, Leicester City na West Ham United zimepewa nafasi ya kumsajili beki huyo huku pia timu kutoka Italia na Ujerumani zikionesha nia.

Related Articles

Back to top button