Panga kali kupita Man United
TETESI za usajili zinaeleza kuwa klabu ya Manchester United inajiandaa kusafisha kikosi mwaka 2024 huku wachezaji 15 wakitarajiwa kuondoka wakati wa uhamisho majira ya baridi na kiangazi.
Winga Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuwa wa kwanza kuondoka mapema mwaka ujao.(MEN/Star)
Newcastle United inamfuatilia Dominic Calvert-Lewin wa Everton wakati mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 25 akiwa kwenye orodha ya usajili ya timu kadhaa zinazomwania majira yajayo ya kiangazi.(TeamTalk)
Fulham inaongoza mbele ya Liverpool na Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo Mbrazil wa Fluminense, Andre mwenye umri wa miaka 22. (Standard)
Manchester City ipo katika jitihada kumshawishi mshambuliaji Erling Haaland mwenye umri wa miaka 23 kusaini mkataba mpya, lakini makubaliano na mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway hayatarajiwi kukamilika hivi karibuni.(TeamTalk)