Bayern yawania saini ya Varane

TETESI za usajili zinaeleza kuwa klabu ya Bayern Munich imefanya majadiliano ya ndani kuhusu usajili wa beki wa kati Raphaël Varane, ambaye siku za hivi karibuni amekuwa sio mchezaji pendwa Manchester United.
Ingawa beki huyo yupo sokoni Januari 2024, Bayern huenda ikashindwa kumudu bei United inayotaka kumuuza.(Sky Sport Germany)
Pia Bayern Munich ina nia kumsajili Takehiro Tomiyasu wa Arsenal lakini tena huenda isikubali vipengele vya uhamisho kabla ya majira ya kiangazi na badala yake itaendelea kumfuatilia.(Sky Sport Germany)
Hata hivyo, Arsenal inapanga kufungua mazungumzo ya mkataba na Tomiyasu katika siku zijazo kufuatia kiwango bora mwanzo wa msimu. (TeamTALK)
Chelsea bado inapima iwapo ivunje benki kumsajili mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney Januari 2024. (football.london)
Atletico Madrid ingekusudia kumuuza moja kwa moja Joao Felix katika klabu ya Barcedona kwa ada ya pauni milioni 60 hadi 70.(MARCA)
Pia Barcelona ingependa huduma ya Joao Cancelo iendelee mara mkopo wake wa awali kutoka Manchester City utakapofikia kikomo. (Football Espana)