Liverpool, Arsenal, City zamgombea Kimmich
TETESI za usajili zinasema Liverpool, Arsenal na Manchester City zinagombea saini ya kiungo wa Bayern Munich, Joshua Kimmich.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 29 anataka kuondoka Bavaria majira yajayo ya kiangazi. (Express)
Klabu yoyote inayotaka kumuajiri kocha mkuu wa Brighton ‘Seagulls’, Roberto de Zerbi majira yajayo ya kiangazi italazimika kuwalipa Seagulls pauni mil 12.8.(Mirror)
Barcelona, Liverpool na Manchester United zimekuwa zikihusishwa kuhitaji huduma ya mtaliano huyo. (Mirror)
Beki wa kihispania Marc Cucurella, 25, anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji kadhaa wenye majina makubwa watakaouzwa na Chelsea majira yajayo ya kiangazi. (Football Insider)
Beki wa kati wa Manchester City na Ureno, Joao Cancelo, 29, anataka kuongeza mkopo wake katika klabu ya Barcelona zaidi ya msimu huu. (Sky Sports)
Liverpool, Borussia Dortmund na Paris St-Germain zina nia kumsajili kiungo wa Argentine Alan Varela, 22, lakini zitalazimika kuilipa FC Porto pauni mil 60 za kipengele chake cha kuachiwa. (Foot Mercato – in French)