Mastaa

nthony Joshua awa kivutio kwa wanawake

BONDIA maarufu wa uzani wa juu duniani, Anthony Joshua, ameibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kushiriki video na picha zinazoonesha upande wake wa kawaida na wa upole akicheza na mbuzi.

Nyota huyo mwenye asili ya Nigeria lakini anayeiwakilisha Uingereza aliweka chapisho kwenye Instagram lililoambatana na maneno ‘Village boy’, jambo ambalo liliwavutia maelfu ya mashabiki wake duniani kote.

Katika picha na video hiyo fupi, Joshua anaonekana akiwa ameketi kwa utulivu juu ya ukingo wa mawe katika mazingira yanayoonekana kuwa ya nje na yenye utulivu. Bondia huyo alikuwa amevalia kaptula nyeusi, viatu vyeupe vya michezo, kofia nyeupe aliyovaa kwa kuigeuza nyuma, huku akiwa amebeba taulo begani na kuvaa mkufu wa dhahabu shingoni.

Muonekano wake wa kawaida na usio wa kifahari uliwafanya wengi kuona upande tofauti wa mwanamichezo huyo ambaye mara nyingi huonekana akiwa kwenye mazoezi makali au katika mapambano makubwa ya ndondi.

Kilichowavutia zaidi mashabiki ni namna Joshua alivyokuwa akicheza na mbuzi huyo kwa umakini mkubwa huku akiwa ameshika simu mkononi mmoja, alionekana akimpapasa mbuzi huyo mwenye rangi nyeupe na mabaka ya kahawia huku akitabasamu.

Mbuzi huyo naye alionekana mwenye utulivu akisimama karibu sana na bondia huyo kana kwamba walikuwa marafiki wa muda mrefu.

Jambo hilo liliongeza mvuto wake kwa mashabiki ambao walifurahia kumuona katika mazingira tofauti na yale ya ulingoni.
Mara baada ya chapisho hilo kusambaa, sehemu ya maoni ilifurika ujumbe kutoka kwa mashabiki, hasa wanawake, waliovutiwa na tukio hilo.

Baadhi yao walitoa maoni ya utani wakisema wangependa kuwa katika nafasi ya mbuzi huyo ili wapate kubembelezwa na Joshua. Wengine walieleza kuwa video hiyo imewaonesha upande wa kuvutia zaidi wa bondia huyo, wakisema kuwa nguvu zake ulingoni zinaendana na upole wake nje ya mchezo.

Mashabiki wengine walimsifu Joshua kwa kubaki mnyenyekevu licha ya mafanikio makubwa aliyoyapata katika maisha yake ya michezo. Kauli yake ya ‘Village boy’ ilitafsiriwa na wengi kama ishara ya kutokusahau alikotoka na kuthamini maisha ya kawaida licha ya kuwa mmoja wa wanamichezo maarufu duniani.

Related Articles

Back to top button