FilamuMastaa

Lupita: Sitamsahau Chadwick Boseman

NEW YORK: ZAIDI ya miaka minne baada ya kifo cha nyota wa Black Panther, Chadwick Boseman kufariki dunia akiwa na miaka 43 kutokana na saratani ya utumbo mpana, muigizaji Mkenya anayeishi Mexico, Lupita Nyong’o ameweka wazi kwamba hatokuja kumsahau msanii huyo licha ya kufariki dunia.

Lupita mwenye tuzo ya Oscar alisema hayo baada ya kuitazama klipu yao wakiwa pamoja katika filamu waliyocheza mwaka 2018 huku akionekana kujawa na huzuni.

“Lazima nikubali, sijaona filamu tangu Chadwick afe, kwa hivyo nina wakati mgumu mno nikiwa natazama video tulizoshoot pamoja,” Lupita alisema kwa hisia aliposhiriki Tamasha la Filamu la BFI London, Oktoba 14.

“Huzuni ni upendo tu usio na mahali pa kuweka. Sikimbii huzuni. Unaishi nayo tu. Hatutotenganishwa na upendo tulionao baina yenu.”

“Ninatazama video hii na nimejawa na huzuni,” aliendelea. “Sijui kama nitawahi kutoa machozi yangu kutokana na kumpoteza rafiki kama ilivyo kwa Chadwick Boseman, nitamkumbuka milele.”

Chadwick alifariki mwaka 2020 akiwa ameshafanya filamu ya Black Panther: Wakanda Forever.

Naye muongozaji wa filamu ya Wakanda, Ryan Coogler alidai kwamba kutokana na Chadwick Boseman kuwa kiongozi kwao wakati wa uhai wao aliamua kuwa anavaa mkufu wenye picha ya Chad kila alipokuwa katika harakati za upigaji picha za filamu zake.

Related Articles

Back to top button