
KUTOKA Kaskazini hadi Nyanda za Juu Kusini mkoani Mbeya, klabu ya Polisi Tanzania leo ni mgeni wa Mbeya City katika uwanja wa Sokoine katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Mbeya City inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 6 wakati Polisi Tanzania ipo mwisho wa msimamo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 2 baada ya michezo 6 pia.
Katika ukurasa wake rasmi wa Instagram Polisi Tanzania imeandika: “Mapambano ya alama tatu rasmi yanaanza leo uwanja wa Sokoine.”
Kwa mara ya mwisho Mbeya City na Polisi Tanzania zilikutana katika mchezo wa Ligi Kuu Mei 15, 2022 zikitoka suluhu katika uwanja wa Sokoine.